Friday, March 25, 2011

UNFAITHFUL HUSBAND


 Inasikitisha,inafurahisha,inafundisha.
 Mke wa Frank anajivunia mume mtulivu, hashindi baa na hatongozi videmu.
Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za dinner. Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani asiyependa starehe japo kidogo?
Mke akamlazimisha outing, Frank akabisha lakini taxi ikafika. Gonga Club & Lodge.

Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita, “Mambo Frank!” “Poa”

“Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu?”
mke akauliza
Yule mgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time hapa” akajibu Frank

Wakachagua meza. Kukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager.

Akamuuliza mama anakunywa nini. Mhudumu alipoondoka mama akauliza,
“amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu?”

Wakati Frank anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba akawa amefika na kuuliza.

“Mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji nitawaletea huko huko”

Kufikia hapo mama akawa hana simile tena, akanyanyuka akitukana kama chizi. Akatoka nje mbio na kuingia katika taxi iliyokuwepo pale.

Wakati anapatana bei na dereva, Frank naye akaingia. Mama
yakamporomoka matusi kibao na kilio juu. Alipovuta kamasi na kupiga kwikwi akamsikia dereve anasema.

“Duh, eee bwana Frank huyu malaya uliyeokota leo balaaaaaaaaaaaaaaa kuliko wa jana!!!!!!”

Mamaa akazimiaaaazzzzzzzzzzzzzzzzzzzz

2 comments:

Anonymous said...

hahahaaaaaaaaaaaaaaaaa!ilike that,so fun

Anonymous said...

mbavu zangu jamani,