Sunday, November 27, 2011

QATAR YAINYIMA VIZA TANZANIA,KOSA NI KUMSAPOTI MUAMAR GADDAF.

Nchi ya Qatar imezuia visa kwa Watanzania,baada ya Serikali ya Tanzania kumsupport Muamar Gaddafi na Kutoitambua Serikali mpa ya Libya. Hii ilionyesha wazi wakati raia wa Watanzania wanaoishi nchini Qatar walipojaribu kuwaombea visa familiya zao walioko huko tanzania. Wananchi hao watanzania waliambiwa kua nchi yenu imezuiwa na haipewi visa. hii ni karibu ya miezi sita sasa toka nchi hio isimamishe viza hizo kwa tanzania lakini hakuna ishara au ufuatiliaji wowote ule uliochukuliwa na Serikali hio ya Tanzania kuweza kutatua tatizo hili.Qatar ni nchi ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi na nchi ambayo inahitaji wafanyakazi kutoka nchi mbalimbali duniani, Qatar tayari huko nyuma ilishakubaliana na Tanzania kuweza kuchukua wafanyakazi kutoka tanzania lakini kwa saga hili lililotokea inaonyesha Qatar itasimamisha kuchukua wafanyakazi kutoka huko na kuchukua wafanyakazi kutoka kenya na nchi nyengine duniani.