HADITHI NJOO UTAM KOLEA.
Hapo zamani za kale alitokea jamaa mmoja katika kijiji chao alisifika kuwa
na roho mbaya sana. Sifa hizo za roho mbaya zikamfikia mfalme
wa kijiji chao. Hivyo katika sherehe kubwa aliyoindaa kwa
ajili ya kusherekea mavuno mfalme akamwalika jamaa na kukaa
nae mezani. Mwisho wa ile sherehe mfalme akamuuliza jamaa
mbele ya hadhira.
Mfalme" kijana naomba uombe kitu kimoja tu. lakini kila
utakachoomba kimoja ndugu yako nitampa viwili zaidi yako"
jamaaa akafikilia sana na akajibu
jammaa" mheshimiwa mfalme naomba nitobolewe jicho langu la
kushoto" . Mfalme akaguna na akasema,
mfalme: " du kweli wewe una roho mbaya hivyo naamrisha
maaskari wakukamate na wakakutupe gerezani. Kwa maana kuwa
ukitobolewa jicho moja nduguyo atatobolewa yote mawili na
nimeamini kuwa una roho mbaya.
Mtu mwenye roho mbaya mwisho wake ni majuto na kuona kuwa
anaonewa. Mwisho wake upo lakini unaweza kuchelewa tu kwa
sababu moja au nyingine. akitendwa huwa analalamika sana.
Regards
No comments:
Post a Comment