Tuesday, December 14, 2010

Anwani isiyo sahihi ya ujumbe wa Kompyuta (e-mail au barua pepe) yazua balaa:


Mwanaume mmoja alifika na kupanga katika hoteli fulani Mjini Unguja. Katika chumba cha hotel yake kulikuwa na Kompyuta, hivyo akaamua kumtumia mkewe barua pepe.
Bahati mbaya akaandika anwani ya barua pepe ambayo si sahihi, na bila kubaini hilo kosa, akaituma barua pepe hiyo.
Wakati huohuo... pahala fulani katika jiji la Mwanza, mwanamke mmoja kizuka alikuwa ndo kwanza amerejea nyumbani toka kwenye mazishi ya mumewe.
Kizuka huyu aliamua kusoma barua pepe zake, akitegemea kusoma barua pepe mbali mbali za kumfariji toka kwa nduguze na mafariki zake.
Baada ya kusoma barua pepe ya kwanza, akapoteza fahamu (akazimia). Mtoto wa kiume wa kizuka huyu akaingia mbio mbio chumbani kwa mama yake, alimkuta mama yake amelala sakafuni, screen ya kompyuta ilikuwa na ujumbe (barua pepe) ulosomeka kama ifuatavyo:
Kwenda kwa: Mke wangu mpendwa
Somo: Nimefika salama
Tarehe: 06 Februari XXXX
Ninafahamu utashangaa kupata ujumbe kutoka kwangu. Hata huku wanazo kompyuta, na tunaruhusiwa kutuma barua pepe kwa wapendwa wetu.
Ndo kwanza nimefika na nimeshapokelewa.
Kwa ujumla kila kitu kimeshaandaliwa ili nawe uweze kuwasili hapa kesho.
Ni matumaini yangu kuwa tutaonana hiyo KESHO!

Bi dada huyo baada ya kupata ujumbe huu ALIZIRAI  !!


1 comment:

Anonymous said...

ha ha ha hahaaaaaa!!!mwe ingekuwa mm nahic ningekufa kabisa hapohapo,ha ha ha haaaaaaaaa